Subscribe to this channel

You can subscribe to new audio episodes published on this channel. You can follow updates using the channel's RSS feed, or via other audio platforms you may already be using.

RSS Feed

You can use any RSS feed reader to follow updates, even your browser. We recommend using an application dedicated to listening podcasts for the best experience. iOS users can look at Overcast or Castro. Pocket Casts is also very popular and has both iOS and Android versions. Add the above link to the application to follow this podcast channel.

Signup to iono.fm

Sign up for a free iono.fm user account to start building your playlist of podcast channels. You'll be able to build a personalised RSS feed you can follow or listen with our web player.
23
SEP

KONGAMANO LA WABUNGE WANAWAKE WA JUMUIYA NA MADOLA NCHINI UGANDA

Spika wa bunge la Uganda afungua rasmi mkutano wa chama cha wabunge wakike katika jumuiya ya nchi za madola

Mwandishi: Monday Akol Amazima

Spika wa bunge la jumhuri ya Uganda Mheshimiwa Rebecca Alitwala Kadaga amewaomba wanaume kuunga mkono shughuli za akina mama. Mh. Kadaga ambaye alikuwa anafungua mkutano wa chama cha wabunge wanawake katika nchi za jumuiya ya madola aliendelea kusema kuwa katika nchi za madola idadi ya wabunge wa kike inaendelea kuongezeka.
Uganda ni mwenye wa mkutano mkuu wa 64 wa chama cha wabunge katika nchi za jumuiya ya madola ambao umeanza rasmi leo tarehe 23 September 2019 na utaendelea hadi tarehe 29. Mkutano huu unahudhuriwa na wabunge kutoka nchi wanachama 53. Mkutano huu ambao ni mara ya pili kufanyika nchini Uganda utakuwa na shughuli kadhaa za wajumbe na matawi ya chama.
Mathalani chama hicho kina umoja wa wanake yaani CWP (Common Wealth Women Parliamentarians Association) ambapo Mh. Rebecca Kadaga ndiye Mwenyekiti. Mara ya kwanza mkutano huu kufanyika nchini Uganda ilikuwa miaka ya sitini ambapo wakati huo wabunge wanawake walikuwa wachache mno.
Spika Kadaga alisema chama cha wabunge wanawake katika nchi za jumuiya ya madola kilianzishwa miaka 30 iliyopita kama sehemu ya chama kikubwa cha CPA yaani chama cha mabunge katika jumuiya ya madola.
Mkutano huu unatarajia kufika kilele siku ya alhamisi ambapo rais Yoweri Museveni wa Uganda ataufungua rasmi kama makamu mlezi wa chama hicho. Mlezi wa chama ni Malkia Elizabeth wa Uingereza.

Mkutano huu unaendelezwa chini ya kauli mbiu, kuzoea, kuhusisha na ukuwaji wa mabunge katikajumuiya ya madola inayobadilika kwa kasi.

896 episodes

« Back 1—12 More »